MTANGAZAJI

PROGRAM TUMISHI YA HOSPITALI YA WAADVENTISTA YASHINDA TUZO NCHINI AUSTRALIA





 San Medical Informatics doctor liaison Bronwyn Gaut presenting at the Health Informatics Conference in Australia in August 2019. [Photo: Adventist Record]

Hospitali ya Waadventista ya Sydney nchini Australia, inayojulikana kwa jina The San, imeshinda tuzo ya heshima kutokana na kutengeneza Program Tumishi inayotoa taarifa za Afya za Wagonjwa kwa Madaktari.

 Program tumishi hiyo ambayo inatoa mwanya wa kuwapatia madaktari taarifa za wagonjwa viganjani imepewa jina la SanCare ambayo imeshinda  tuzo ya shindano la Jumuia ya Taarifa za Afya ya nchini Australia (HISA) kwa mwaka 2019.

Daktari wa San anayehusika na taarifa za kitabibu na Mahusiano  Brownyn Gaunt akiwa na wataalamu wa huduma za taarifa waliionesha program tumishi hiyo kwenye Kongamano la  HISA mjini Melbourne Agosti 12-14.

SanCare ilibuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa taarifa za Afya kwa ajili ya kuwapatia madaktari muda muafaka wa kupata taarifa za wagonjwa,dalili za ugonjwa,vipimo mbalimbali vikiwemo x-ray,scan na matokeo ya vipimo na kuwasiliana na wahudumu wa afya.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.