RAIS KAGAME ASHIRIKI UZINDUZI WA CHUO KIKUU CHA AFYA CHA WAADVENTISTA (+VIDEO)
Rais wa Rwanda Mh,Paul Kagame akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson kwa pamoja wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi,mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa chuo hicho leo mjini Kigali,nchini Rwanda. |
Mwenyekiti
wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Mch.Ted Wilson
na Rais wa Rwanda wameshiriki katika uzidunzi wa Chuo Kikuu cha Afya nchini Rwanda kwa lengo la kutoa Elimu ya Afya kwa wanafunzi wa Afrika Mashariki na Kati
Hafla
fupi ya uzinduzi wa chuo hicho cha afya kinachomilikiwa na Kanisa la
Waadventista wa Sabato katika Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) limefanyika Septemba 2 mwaka huu mjini
Kigali ambapo Mch Ted Wilson amesema elimu bora siyo jengo bali ni huduma
bora inayotolewa ndani ya majengo hayo huku akisema chuo hicho licha ya
kutoa elimu ya afya inatoa huduma ya kiroho.
Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwa kutambua huduma mbalimbali
zinazotolewa na kanisa hilo, Serikali yake itaongeza ardhi kwa chuo
hicho pamoja na fedha, huku akipongeza Makanisa ya Waadventista wa Sabato
nchini humo kwa kuadhimisha miaka 100 ya utoaji huduma ya kijamii na
kiroho nchini Rwanda,kwani huduma walizozitoa zimekuwa na matokeo
makubwa katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya afya na elimu.
Awali
akiwasilisha taarifa fupi ya chuo hicho Mwenyekiti wa jimbo la Afrika
Mashariki na kati Mchungaji,Dkt Blasous Luguri alieleza kuwa mpaka
kukamilika kwa ujenzi wa chuo hicho, kitasaidia kutoa mchango mkubwa wa
elimu ya afya nchini humo.
Uzinduzi
wa chuo hicho umeshuhudiwa na viongozi wa Serikali ya Rwanda akiwemo
Waziri wa Afya nchini humo Diana Lumba, Waziri wa Elimu Eugene Tamura
pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa la Waadventista wasabato
divisheni ya Afrika.
Post a Comment