MTANGAZAJI

TIMU ZA WATAFUTA NJIA WA KANISA LA WAADENTISTA HOUSTON INTERNATIONAL ZASHINDA SHINDANO LA USOMAJI WA BIBLIA (+VIDEO)                                                                 His Hikers Jericho


                                                            His Hikers Jordan

                                                                 His Hikers Judea


Timu  tatu za Kanisa la Waadventista wa Sabato la Houston International zimeshika nafasi ya kwanza  kwenye  mashindano ya usomaji wa Biblia  kwa Vijana wa Chama cha Watafuta Njia wa Divisheni ya Amerika ya Kaskazini (NAD) mwaka 2019 yenye Kauli Mbiu ya "Watafuta Njia,Uzoefu wa Biblia"yaliyofanyika April 26 hadi 27 mwaka huu katika Chuo cha Rock Valley,RockFord,Illinois,Marekani.

Timu hizo zilizokuwa miongoni mwa timu  209 toka katika Unioni zipatazo 10 zilizoko katika nchi za Marekani,Canada na Uingereza ambapo makanisa yaliyoko kwenye Jimbo la Texas lililoko  katika Unioni ya Kusini Magharibi likiwa na timu 23 ni His Hikers Jordan,His Hikers Jericho  na His Hikers Judea.

Mashindano ya usomaji wa Biblia yamekuwa yakifanyika katika Divisheni hiyo  kila mwaka kwa muda wa zaidi ya miaka 10 sasa.

Vikundi ama timu za watafuta njia wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 hushiriki  kwa njia ya mchujo kuanzia Kanisa,Mtaa,Konferensi na Unioni  na vinavyoshika nafasi ya kwanza huambatana na walimu,wazazi ama walezi kwenye mashindano ya ngazi ya Divisheni ambapo kwa mwaka huu takribani Watafuta Njia 4000 walishiriki na kuulizwa maswali 90 kutoka katika kitabu cha Luka na vitabu vya Roho ya Unabii vya Kanisa hilo ambavyo hufafanua Biblia kwa undani.


Mashindano ya mwaka huu yalihitimishwa kwa Hotuba toka kwa Mkurugenzi wa Watafuta Njia Ulimwenguni Andres Peralta aliyewataka vijana hao kujitambua na kufahamu thamani yao katika maisha  na kisha  utoaji wa vyeti kwa washindi huku Uingereza ikiongoza kuwa na washiriki wengi zaidi,mashindano ya mwaka 2020 yatahitimishwa katika jiji la Washington nchini Marekani.
   

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.