UONGOZI WA IDARA YA HUDUMA ZA VIJANA KANISA LA WAADVENTISTA WAVUTIWA NA MASHINDANO YA USOMAJI WA BIBLIA (+VIDEO)
Uongozi wa Idara ya Huduma za Vijana ya Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) umeeleza kuwa unatamani pia kuanzisha mashindano ya kusoma Biblia kwa vijana wa Chama cha Watafuta Njia katika eneo hilo.
Mchungaji Magulilo Mwakalonge ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Vijana ECD eneo linalojumuisha nchi 11 aliyeshuhudia mashindano ya Usomaji wa Biblia ya mwaka huu ya Divisheni ya Amerika ya Kaskazini (NAD)yaliyopewa Kauli Mbiu isemayo "Watafuta Njia,Uzoefu wa Biblia"ambayo yalifanyika katika Uwanja wa ndani wa Chuo cha Rock Valley,Rockford,Illinois Marekani amesema kuna haja ya kuweka mikakati ya kufanyika kwa mashindano hayo kwa nchi za Afrika kwa kuwa yanawafanya watoto waweze kuwa na misingi bora ya kuifahamu Biblia kwa faida yao na kanisa hilo kwa ujumla.
Takribani watoto 4000 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 15 walishiriki mashindano ya Divisheni ya mwaka huu ambao walipatikana kuanzia katika ngazi ya Kanisa,Mtaa,Konferensi,Unioni na mwisho katika ngazi ya Divisheni ambapo jumla ya Unioni 10 za NAD zenye vikundi (timu) 209 toka katika nchi za Marekani,Canada na Uingereza zilishiriki huku yakiulizwa maswali 90 kutoka katika kitabu cha Luka na vitabu vya Roho ya Unabii vya Kanisa hilo ambavyo hufafanua Biblia kwa undani.
Divisheni ya Amerika ya Kaskazini imekuwa ikifanya mashindano hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa ambapo vikundi vya watafuta njia vilivyoshiriki katika ngazi za mchujo na kushika nafasi ya kwanza huambatana na walimu,wazazi ama walezi kwenye mashindano ya ngazi ya Divisheni,mashindano ya mwaka 2020 yatahitimishwa katika jiji la Washington nchini Marekani.
Post a Comment