MTANGAZAJI

WANANCHI WA ROMBO WASHUKURU HUDUMA ZA UPIMAJI WA AFYA BURE TOKA KWA ATAPE


Mmoja wa wakazi wa Rombo Kilimanjaro akipatiwa huduma ya vipimo vya Afya
Moja ya Kituo kichaotumiwa na ATAPE kuendesha huduma za upimaji wa Afya Bure huko Rombo
Huduma ya Upimaji afya bure katika Wilaya ya Rombo  inayoratibiwa na Chama cha Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista  (ATAPE ) inaendelea katika vituo vitatu vya Rombo Mkuu,Keni na Mokoro-Useri.
Huduma hii ambayo ilizinduliwa Rasmi mapema Februari 9,2019  imekuwa na mvuto  kwa jamii ya wakazi wa Rombo hasa kituo cha Mokoro Useri.
 Diwani wa kata ya Kingachi Daudi Mlasani Tarimo kamewatangazia wananchi wake kuhudhuria kushiriki  kupima afya zao kwani huduma kama hii haijawahi kufanywa bure katika eneo hilo.

Pia amewatangazia wananchi Wote kuhudhuria na kusikiliza Mahubiri ya Nyumbani hatimaye maana katika kusikiliza ndipo mtu anaweza kuamua.
Huduma  ya kupima afya bure kwa wakazi wa Rombo inahusisha vipimo vya Magonjwa ya shinikizo la damu, kisukari, uzito ,huduma ya Macho, HIV na  Ushauri nasaha.
Baadhi ya wakazi wa Rombo wakizungumza na vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista nchini Tanzania,Hope Channel Tanzania na Morning star Radio wameeleza kuwa katika eneo hilo ni Mara ya kwanza kupatiwa huduma hizi za afya bure ambao wamepongeza juhudi za Wanataaluma Waadventista Wa Sabato Tanzania kuratibu Mkutano  wa Nyumbani Hatimaye ambapo waeahidi kuhudhuria kila siku.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.