MTANGAZAJI

KWAYA YA WAADVENTISTA UBUNGO HILL KUTOKA FAMILIA HADI NYUMBANI HATIMAYE 2019 (+VIDEO NA PICHA)

Waimbaji wa Kwaya ya Ubungo Hill wakiimba kwa Mkutano wa Nyumbani 2019 unaorushwa mbashara Hope Channel Tanzania na Morning Star Radio kutoka Kinyerezi ,hapa ilikuwa ni Februari 9,2019
Mwimbaji wa Sauti ya Kwanza Ester Mwakalinga
Unapozungumzia kwaya ambazo zimeendelea kudumu katika aina yake ya uimbaji kwa muda mrefu katika jiji la Dar es salaam,Tanzania ni kwaya ya Ubungo Hill ya Waadventista wa Sabato ambayo ilianzishwa na waimbaji wa familia tano mwaka 1986.

1.Familia ya Amosi Mwakalinga ambao pia waliwahi kuimba na kwaya ya Ushindi-Mikocheni B huku mtoto wao kike Ester Mwakalinga ambaye ni mwanasheria akiwa ni mwimbaji wa sauti ya kwaya katika kwaya ya Ubungo Hill mpaka sasa
2.Familia ya Jacob Mwangake
3.Familia ya Andambike Mwaipopo
4.Familia ya Mwalubandu 
5.Familia ya Nasion Busee 
Familia hizi zilikuwa zikiabudu katika majengo ya Shule Msingi Ubungo Kisiwani wakati huo.
Ambapo mwalimu wao alikuwa ni Mwakyosa na Ibrahim Frank.

Mwaka 1995 ndipo ilipopata nguvu na kuimarika zaidi kwaya hii huku Kwaya ya Waadventista Magomeni Mwembechai ikisaidia maendeleo ya Ubungo Hill ambapo walipeleka walimu kufundisha kwaya hii ambao ni Daniel Mwambene na Mapesa Kambira aliyeko Marekani huku mdogo wake Lugora Kambira  akiwa bado ni miongoni mwa walimu na waimbaji wa Kwaya ya Ubungo Hill mpaka sasa (Angalia video yao hapa)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.