MABORESHO SHERIA MPYA YA MADINI, MAJENGO NA VAT YAFANYWA NA BUNGE LA TANZANIA
Bunge limepitisha Muswada wa Sheria wa Marekebisho ya
Sheria mbalimbali Namba mbili ya Mwaka 2019 ambao umelenga kutatua changamoto
za za kodi ikiwemokodi ya Majengo, madini na Kodi uya Ongezeko la Thamani
(VAT).
Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa Hati ya Dharura
ulijadiliwa na kupitishwa ambapo Wabunge
mbalimbali walipata fursa ya kutoa maoni yao.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha Muswada huo, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mhe. Prof. Adelardus Kilangi, alisema kuwa marekebisho hayo yameondoa kodi ya zuio (withholding tax) kutoka 5% hadi asilimia
sifuri kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji wadogo ili
kuwahamasisha wachimbaji hao kuuza madini katika masoko ya madini.
Amesema marekebisho hayo yanalenga kudhibiti
upotevu wa mapato ya Serikali na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya madini
yanakusanywa ipasavyo.
Muswada huo umependekeza kutoa
msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wachimbaji wadogo wa madini
watakaouza madini yao katika masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini.
Prof. Kilangi alibainisha kuwa Muswada huo
pia umependekeza kila
kiwanja kitozwe Kodi ya Majengo badala ya kila jengo lililopo ndani ya kiwanja
husika kwa maeneo ya Halmashauri za Wilaya.
Sheria
zilizopitishwa ni pamoja na Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147, Sheria ya Kodi ya Mapato Sura ya 332, Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Utozaji
wa Kodi ya Majengo Sura ya 289, Sheria ya Madini Sura ya 123 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani Sura ya
148.
Post a Comment