RIPOTI YAONESHA MGONJWA ALIFARIKI BAADA YA KUWEKEWA DAMU ISIYO YA GROUP LAKE
Ripoti ya Uchunguzi uliofanywa katika Hospitali ya St Luke iliyopo Houston Marekani imeonesha kuwa mgonjwa aliyefariki mwezi Disemba mwaka jana aliwekewa damu ya group ambalo si lake hali iliyosababisha kifo chake.
Mwanamke huyo aliyekuwa na damu ya group B+ alifika hospitalini hapo mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana akiwa na tatizo la kuvujia damu katika ubongo wake kisha akawekewa damu ya group A+ na baada ya hapo akapata shinikizo la damu ndani ya masaa matatu na kisha kupoteza maisha siku iliyofuata.
Post a Comment