MTANGAZAJI

FILAMU MPYA ILIYOTENGENEZWA NA WAADVENTISTA KUZINDULIWA (+VIDEO)




Filamu Mpya ya iliyopewa jina la Maisha ya Daniel itazinduliwa rasmi kwenye Mkutano wa Wadau wa Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani (GAiN) unaofanyika Amman, Jordan ukitarajiwa kumalizika Februari 28,mwaka huu.

Filamu hiyo iliyotengenezwa katika mji mdogo maalum kwa masuala ya filamu uitwao  Ouarzazate ulioko katika jangwa la Sahara nchini Morocco kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 8, 2018  ikisimamiwa na taasis nne za habari za kanisa hilo,wataalamu wanane toka nchi tano katika mabara manne duniani, watalaamu wa masuala ya uzalishaji toka Morocco na waigizaji 165 waliobobea katika uhusika uliojikita kwenye mafundisho ya Biblia.

Quarzazate ni mji ambao unajulikana kutokana na kuwa na eneo maalum kwa ajili ya watengenezaji wa filamu toka sehemu mbalimbali duniani ambao hupendelea kutengeneza filamu zenye maudhui toka katika Biblia ama maudhui ya kihistoria.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.