MWIMBAJI WA BASS WA SONDA YA DIHLU FABIAN WEREMA "MR BASS" AJA KIVINGINE (+VIDEO)
Fabian Werema |
*Mianzo*
FabianWerema anaanza kuifahamisha mtangazaji.com kuwa karama ya uimbaji ilikuzwa na mama yake mzazi kupitia Kwaya ya Waadventista ya Kitunda jijini Dar es salaam mwaka 2005 akiwa ni mwimbaji wa sauti ya tatu
Iliopofika mwaka 2012 alihamia mkoa wa Mara kwa ajili ya masomo katika Shule ya Sekondari ya Ikizu inayomilikiwa Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Tanzania na hapo akiwa na waimbaji wengine wanne walianzisha kikundi cha uimbaji wa nyimbo za injili kwa mtindo wa Acappella akiwa ni mwimbaji mwongozaji.
Fabian anaeleza kuwa mwaka 2014 alirudi jijini Dar es salaam Dar es salaam na kutafuta kundi la kujiunga nalo katika uimbaji.
"Kuna siku nilikuwa nasikiliza mahojiano kwa Morning Star Radio ya kikundi cha Sauti ya Matumaini ambacho kwa sasa hakipo, ila nilivutiwa nao na walipotoa mawasiliano nilichukua namba na kuomba kujiunga nao,nilifanikiwa kujiunga kama mwimbaji wa sauti ya pili" anasema Mr Bass
*Kutoka Sauti ya 3,1,4 hadi Bass*
" Siku moja nilikuwa najaribu kuimba wimbo wa Sonda ya Dihlu nikiwa na kundi la Sauti ya Matumaini kwa sababu Sabato hiyo tulikuwa tumealikwa pamoja, ghafla mwimbaji mwenzangu Frank Msirikali alinisikia na kuniambia mbona kama unafaa zaidi ukiimba Bass nikacheka tu."anaeleza
*Kutoka Sauti ya Matumaini hadi Sonda ya Dihlu mwaka 2014*
Fabiani anasema siku waliyokutana na Sonda ya Dihlu katika Kanisa la Machimbo alifanikiwa kuimba Bass, Ndipo mwimbaji wa solo wa Sonda ya DiHlu kwa wakati ule Jackson Fanuel akanikaribisha kwenye mazoezi,aliomba kujiunga na Sonda ya Dihlu na akakubaliwa kuwa mwimbaji wa sauti ya pili na Bass japo muda mwingine inapobidi huwa anaimba kidogo sauti ya kwanza.
*Jina Mr. BASS *
"Mwaka 2017 nikiwa chuoni pamoja na roommate wangu Salim, nilimuomba ani rekodi clip fupi ninayoweza kuweka mtandaoni, alifanya hivo na mwishoni kama utani akasema "hebu hakikisha kazi yako kwanza Mr. BASS kabla sijaondoka"anasema
"hafla wazo likanijia kwanini nisilitumie hili jina kama utambulisho wa kazi zangu, ndipo rasmi nikaanza kufahamika kama Mr. BASS kupitia video clip zisizozidi dk 1 Ikiwemo wimbo wa Turn your Radio on, Swing Low Sweet Chariot na nyinginezo"
"Katika hali isiyotarajia mwaka 2018 mwezi Februari katika mikutano ya Maisha Hatimaye iliyokuwa ikifanyika mkoani Mbeya chini ya ATAPE ikirushwa mbashara kupitia Hope Channel Tanzania na Morning Star Radio akiwa na Sonda ya Dihlu katika kipindi cha Lulu za injili Mtangazaji aliendesha kipindi hicho Maduhu Emanueli aliniulizia "Mr.BASS! Kwanini unajiita Mr.BASS" nami nikamjibu "kwa sababu Mungu amenibariki kuwa na Bass"
Hiyo ndo siku ambapo mahojiano hayo yaliiwafikia watu wengi waliokuwa wakifatilia mahubiri hayo na ndipo jina hili likaongezeka thamani maradufu" anaeleza.
*Mr. BASS Music*
Anasema mwaka 2018 pia mwanzoni alipokea ushauri kutoka kwa watu akiwemo Salim, kwamba niache room videos zisizo na ubora na ajaribu kufanya hii kazi katika ubora,na ndipo alipoingia studio na kurekodi na kuanza kazi kwa slogani ya Mr. BASS MUSIC Series #Mzikimtamunisasa na kuachia nyimbo tatu.
Fabian anaeleza kuwa mkakati wake ni kuimba nyimbo zenye ujumbe wenye matumaini, Faraja, onyo, upendo , burudisho na kutumia karama na sanaa kufikisha ujumbe unazoelekeza katika madili mema na kumuheshimu Mungu
Post a Comment