MTANGAZAJI

WANATAALUMA NA WAJASIRIAMALI WAADVENTISTA WAZINDUA HUDUMA YAKUPIMA AFYA BURE WILAYANI ROMBO







Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista nchini Tanzania (ATAPE) kimezindua huduma ya Upimaji afya Bure katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.

Huduma hii imezinduliwa rasmi Februari 9,2019 ikiwa ni sehemu ya  na semina za Nyumbani Hatimaye 2019 zinazoendelea katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kinyerezi Jijini Dar es salaam na kuonekana duniani kote .

Tukio hili limeongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rombo  Abubakar Asenga ambaye alisisitiza wakazi wote wa wilaya ya Rombo kujitokeza kupima afya zao ili wapate matibabu na Ushauri bure.

Katika tukio hili zaidi ya watu mia Tano walihudhuri.Huduma hii ambayo itaendelea kufanyika kuanzia kwa muda wa juma moja.


Huduma hii inatarajiwa kufanyika katika vituo vitatu  ambavyo ni Rombo Mkuu,Keni na Useri.Lengo la huduma ikiwa ni  hii ni kuigusa jamii yenye mahitaji ya afya na ushauri.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.