SERIKALI YA TANZANIA YAELEZA ITAKAVYOTATUA CHANGAMOTO KWA WAGENI WANAOINGIA NCHINI KUPITIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA)
Serikali ya Tanzania kupitia
wizara zake nne tofauti imetoa taarifa ya jinsi itakavyokabiliana na changamoto mbalimbali za
utoaji wa huduma kwa wageni wanaiongia na kutoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere (JNIA) jijijini Dar es Salaam.
Changamoto hizo
ni pamoja na msongamano na joto katika eneo la kuchukuliamizigo, muda mrefu wa
upatikanaji wa hati za kusafiria kwa wageni wanaoingia nchini pamoja na
changamoto ya ufinyu wa eneo la kusubiri huduma uwanjani hapo.
Mawaziri wa
Wizara hizo ambao wamefanya ziara ya pamoja katika uwanja huo jana na kukagua
shughuli za utoaji huduma ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk.Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje Dk.Susan Kolimba na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano,
Mhandisi Atashasta Nditiye.
Akizungumza
uwanjani hapo, Dk. Kigwangalla alisema wamefikia hatua ya kukutana mawaziri hao
baada ya wageni hasa watalii wanaiongia nchini kulalamika kuwa wanatumia muda
mwingi kuhudumiwa katika eneo la uwanja huo kiasi cha kuwapotezea muda.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi
Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana wakati
wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni
hususan watalii wanaoingia nchini
kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine
walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa
pili kulia), Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(wa tatu kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba (wa nne kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Susan Kolimba jijini Dar es salaam jana wakati wa ziara ya pamoja ya kukagua Changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wageni hususan watalii wanaoingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam JNIA kwa ajili ya kukabiliana nazo. Wengine walioshiriki ziara hiyo ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) .
Post a Comment