MTANGAZAJI

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA KITUO CHA MAFUNZO MAALUM YA KIJESHI KILICHOPO MAPINGA MKOANI PWANI

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto anayevuta utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto ni Balozi wa China nchini Tanzania  Wang Ke.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya ufunguzi wa kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la watu wa China.

 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara baada ya kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.