WACHUNGAJI WAASWA KUWA NA IMANI KUBWA KWA MUNGU
Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika Kanda ya Afrika Mashariki na kati Dkt Blasious Ruguri amewaasa wachungaji wa kanisa hilo kuwa na
Imani kubwa kwa Mungu kwani amewapa mamlaka ya kufanya hivyo kama
watumishi wake wake duniani.
Dkt Ruguri Ameyasema hayo katika mkutano wa mwishoni mwa mwaka unofanyika kwenye ofisi za jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania la Waadventista Wa Sabato jijini Arusha ambapo atakuwa na siku mbili za kuzungumza na viongozi wa Jimbo hilo la kaskazini, ambao ni pamoja na maofisa watatu wa jimbo hilo Daktari Godwin Lekundayo(Mwenyekiti),Mchungaji Daudi Makoye(Katibu),Dickson Matiko(Muhazini)
Mkutano huo umejumuisha maofisa watatu wa kila jimbo dogo linalounda Jimbo hilo,wakurugenzi wote wa idara katika ofisi kuu za jimbo pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali za kanisa zilizopo jimboni humo.
Lengo la mkutano huo unaofanyika kila mwaka ni kutathmini utendaji kazi kupitisha bajeti kwa ajili ya matumizi ya mwaka unaofuata wa 2018.
Post a Comment