WAZAZI WATAKIWA KUTOWATENGA WATOTO WENYE ULEMAVU
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anacheza ngoma ya kimasai pamoja na baadhi ya wamasai waliojitokeza katika sherehe za kupandisha ngazi ya rika kutoka katika rika la kurianga kuingia katika rika la Nyangulo (Habari picha na woindeshizza blog )
Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Mollel akiwa anasalimia na moja na mzee aliyekuwa rika la kurianga ambae kwa sasa ameingia katika rika la Nyangulo
Wazazi hususani wa jamii ya kimasai
wametakiwa kuachana na dhana ya kuwatenga na kutowapeleka shule watoto wa kike
na wale ambao ni walemavu badala yake
wawapeleke mashuleni kwani wao ndio viongozi wa baadae
Hayo yamebainishwa na mbunge wa viti
maalumu (CCM) Amina Mollel wakati alipokuwa
akizungumza katika sherehe za kupandisha ngazi rika kutoka katika rika la kurianga
kuingia katika rika la Nyangulo ,sherehe ambazo zilifanyika katika Kijiji cha
Oldenderet Kata ya Nduruma mkoani Arusha
Alisema kuwa kunabaadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wao kisa ni walemavu jambo ambalo
linawakosesha haki zao ikiwemo ya kupata elimu
kutokana na kufichwa huko.
Pia amewataka wazazi wa jamii ya kimasai na hata
wale wa makabila mengine kuacha kuwaozesha watoto wakike mapema kwani watoto
hao wakike nao wanahaki ya kupata elimu kwani elimu ni bure ,kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari hivyo ni vyema
kama wazazi wakawasimamia watoto hususa ni wakike wakaenda shule
Alisema kuwa kunabaadhi ya watoto wa kike wamekuwa wanaacha
kusoma kisa wanakimbilia maisha kitu ambacho sio kizuri kwani wanaweza
kukimbilia maisha yakawapiga hivyo ni muhimu sana kama watasoma kwanza alafu
maisha watayapata baadae baada ya kumaliza kusoma na kupata kazi zao nzuri
Post a Comment