MAKAMU WA KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ULIMWENGU AELEKEA KAHAMA,SHINYANGA
Makamu wa Kiongozi Mkuu
wa Kanisa la Waadventista Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana
anatarajiwa kuhutubia mamia ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato
mjini Kahama kwenye mkutano wa Makambi ya kanda ya Kahama yaliyoanza leo jioni.
Mchungaji Mbwana
anayetokea yalipo makao makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato
Maryland,Marekani amekuwepo nchini toka juma lililopita alipokuwa akihutu
kwenye Makambi ya Musoma Mjini yaliyokuwa yakihudhuriwa na watu wazima wapatao
10,000 na watoto 5,000 yaliyofungwa mjini humo jana.
Makambi ya Kanda ya
Kahama ambayo yamepewa Kauli mbiu ya Kuutwaa Ushuhuda wa Shahidi Mwaminifu yanatarajiwa kurushwa mbashara na Morning Star
Radio pamoja na Morning Star Televisheni yatakuwa yakihudumiwa na wachungaji
watano wakiwemo Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo Kuu la
Kaskazini (NTUC) Dkt Godwin Ole Lekundayo na Mwenyekiti wa Kanisa hilo jimbo la
Nyanza Kusini Mchungaji Sadoki Butoke.
Kwaya zinazotarajiwa
kuhudumu kwenye Makambi hayo yanayofanyika katika viwanja vya Kanisa la
Waadventista Wa Sabato Nyahanga ni ,Nyasubi,Kahama,Nyahanga
Mjini,Majengo,Shunu,Malunga,Igomelo,Mbulu,Buzwagi,Busaka,Mhungula na Mhongolo
Post a Comment