MTANGAZAJI

ZIARA YA WAIMBAJI WA THE LIGHT BEARERS TOKA TANZANIA NCHINI MAREKANI IMEWADIA


Waimbaji wa The Light Bearers toka Dar es salaam,Tanzania watafanya ziara yao ya kiinjilisti ya kwanza nchini Marekani mwaka huu wa 2017 na kuimba katika makanisa mbalimbali nchini humo.

 Septemba 3-23 watakuwa katika Mkutano wa Injili katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Mount of Blessing huko Minnesota,Septemba 25 -30 kwenye juma la Uamsho katika Kanisa la Waadventista Umoja Central la Raleigh huko North Carolina,Oktoba 2-7 watakuwepo kwenye Kanisa la Waadventista Wa Sabato Maranatha huko New Jersey,kisha wataelekea Alabama na kuhitimisha ziara yako huko Houston,Texas kwa Kanisa la Nations of Praise Oktoba 10-14,2017. 

Mwaka jana The Light Bearers walifanya ziara nyingine kama hii huko nchini Uingereza ambako walishiriki kwa mkutano wa Injili na kufanikiwa kurekodi matoleo yao mpya ya santuri mwonekano zilizoko sokoni hivi sasa ikiwemo toleo namba 4.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.