MAKAMU WA KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO DUNIANI MCH GEOFREY MBWANA AWASILI MUSOMA KWA MAKAMBI
Makamu wa Mwenyekiti wa Kanisa La Waadventista Wa Sabato Duniani Mch .Geofrey Mbwana akitoa Marekani yalipo makao makuu ya Kanisa hilo amewasili jana mjini Musoma katika uwanja wa ndege Mjini Musoma Mkoani Mara ambapo ni Mgeni Rasmi na Mnenaji mkuu wa mkutano wa makambi ya mitaa Mitano ya mjini humo.
Mkutano huu unatarajiwa kukusanya zaidi ya waumini elfu 10,000 kutoka katika makanisa mbalimbali ya Waadventista wa Sabato Musoma mjini na nje ya mji huo.
Kiongozi huyo ambaye ni Mtanzania amepokelewa na Mwenyekiti wa kanisa hilo Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania Mch, Dkt. Godwin Lekundayo, Mhazini Mkuu Dickson Matiko, Mwenyekiti wa jimbo la Mara Mch. Ezekiel Ojwan'g,Katibu Mch Enoch Marwa Sando wakiongozwa na vikosi mbalimbali vya watafuta njia.
Mkutano huu ulioanza Agosti August 13 mwaka huu utahitimishwa Agosti 20 mwaka huu na unafanyika katika viwanja vya Kanisa la Waadventista wa Sabato Nyamatare.
Post a Comment