MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:RAIS WA TANZANIA AWATAKA WATANZANIA KUONDOA TOFAUTI ZAO NA KUJENGA NCHI

Rais Mteule Dr John Pombe Joseph Magufuli, ameapishwa leo Novemba 5,2015  kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Magufuli kutoka chama tawala cha CCM, ameapishwa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu ambapo alipata asilimia 58.46 ya kura zote, akimshinda mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa aliyepata asilimia 39.97 ya kura. 

Sherehe za kuapishwa kwa Dr. Magufuli,zimefanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na zimehudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali  Duniani akiwemo Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambapo Dr Magufuli amewataka wananchi kwa ujumla kufuta tofauti zao ili kuijenga Tanzania Mpya.

Kuapishwa kwa rais Magufuli kumeiingiza taifa la Tanzania katika historia ya kuwa na Makamu wa rais wa kike  Mhe Samia Suluhu Hassan kutoka visiwani Zanzibar,tangu taifa hili kupata uhuru.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.