MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:RAIS MAGUFULI AMTEUA GEORGE MCHECHE MASAJU KUWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA




 Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemteua George Mcheche Masaju (Pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ataapishwa leo Novemba 06, 2015  Ikulu Dar es Salaam.

George Masaju  si mgeni kwenye nafasi hiyo, kwani  alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyomaliza muda wake jana Novemba 5,2015  iliyoongozwa na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ambapo aliishika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anaongoza wakati huo, Jaji Frederick Werema kujiuzulu December 2014 wakati wa sakata la ESCROW.

 Taarifa ya Ikulu ya jana mchana ilieleza kuwa Rais Magufuli ameitisha bunge Novemba 17,mwaka huu ambapo atapendekeza jina la Waziri Mkuu wa Tanzania Novemba 19 mwaka huu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.