MTANGAZAJI

CHINA YARUHUSU WAZAZI KUWA NA WATOTO WAWILI
Uchina imeamua kusitisha sera yake iliyodumu miaka mingi ya kuzitaka familia kuwa na mtoto mmoja pekee, shirika la habari la  Xinhua limeripoti.

Familia sasa zitaruhusiwa kuwa na watoto wawili  ambapo sera hiyo tata ilianza kutekelezwa mwaka 1979, ili kupunguza ongezeko la watu nchini humo.

Hata hivyo, kumekuwepo na wasiwasi kutokana na kuwepo sehemu kubwa sana ya raia wazee kwa umri.

Sera hiyo ya kuzaa mtoto mmoja pekee inakadiriwa kuzuia watoto 400 milioni kuzaliwa tangu ianze kutekelezwa.
 
Waliokiuka sera hiyo waliadhibiwa ambapo baadhi yao  wakitozwa faini na kufutwa kazi na hata kulazimishwa kutoa mimba.

Kadri siku zilivyosonga, sera hiyo ililegezwa katika baadhi ya mikoa, huku wataalamu kuhusu idadi ya watu na masuala ya kijamii wakieleza wasiwasi kutokana na ongezeko la gharama ya kuwatunza watu wazee na kupungua kwa idadi ya watu wanaoweza kufanya kazi.
 
Chama cha Communist Party kilianza rasmi kulegeza sharia hiyo miaka miwili iliyopita, na kuwaruhusu wachumba ambao mmoja wao hana ndugu kuzaa mtoto wa pili.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.