SIKILIZA SABABU 14 ALIZOZIELEZA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI TANZANIA (NEC) ZA KUENDELEA KWA TUME KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA BARA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI WA ZANZIBAR KUFUTWA
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (pichani) ametoa sababu 14 ambazo zinafanya tume hiyo iendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar hii leo.
ZEC imetangaza leo kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar na Wawakilishi na kueleza kupitia Mwenyekiti wa Tume hiyo Jecha Salim Jecha kuwa utarudiwa baada ya siku 90.
Awali leo Oktoba 28 asubuhi Jaji Lubuva alieleza sababu za NEC kuendelea kutangaza matokeo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama walivyoanza Oktoba 26,2015,na kufafanua kuwa Tume haiko tayali kufanya marumbano na wanasiasa.
Post a Comment