DAR ES SALAAM:WANAWAKE WANAOUGUA KANSA YA KIZAZI NCHINI TANZANIA KUPATA MATIBABU BURE
Wanawake wanaougua maradhi ya kansa ya kizazi
nchini Tanzania wamepunguziwa adha ya kusumbuka na gharama za matibabu zinazo wakabili.
Vodacom Foundation kupitia kwa Mkurugenzi wake Renatus Rwehikiza anasema
ugonjwa wa kansa ya kizazi umekuwa tishio nchini Tanzania na umesababisha vifo vya
akinamama wengi na kufikia asilimia 38.4
ukiondoa wagonjwa wa kansa za aina nyingine hivyo taasisi hiyo imetoa
kiasi cha dola za Marekani 87,400 kwa
ajili ya kuwawezesha kina mama kwa kuwaleta katika taasisi ya uchunguzi na
matibabu ya kansa ya Ocean Road kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kupatiwa
matibabu.
Amesema Tanzania pia ni nchi yenye
vifo vingi vinavyotokana na kansa barani
Afrika,hivyo lazima magonjwa tishio nchini yatiliwe mkazo ili kutokomeza na
kunusuru wananchi kutokana na vifo vinavyotokana na ugonjwa huu.
Post a Comment