PICHA:ULIVYOKUWA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA KUPITIA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa unaoundwa na vyama vinne, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani jana Agosti 29 mwaka huu.Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani jana
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jana katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani jana.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.
Halima Mdee akihutubia
Wagombea Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jana zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar Waliojitokeza jana katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani jijini Dar
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani jana
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa
Moja ya kifaa cha Kisasa kabisa aina ya Drone ambacho kilikua kikitumika kupiga picha kutoka anagani ambacho kimekuwa kivutio kikubwa kabisa kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam jana katika viwanja vya jangwani .Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Post a Comment