MTANGAZAJI

MANYARA:AKAMATWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MENO YA TEMBOJeshi la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Lemnyake Mbaile mwenye miaka 63 mkazi wa Kijiji cha Makame Wilayani Kiteto Mkoani Manyara kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo. 

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Kamishna Msaidizi Wa Jeshi La Polisi Christopha Foime amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo mahojiano baina yake na jeshi la polisi yakikamilika atafikishwa mahamani kujibu mashtaka yanayomkabili. 

Kamanda Foime amesema walipata taarifa hizo na kuweka mtego kisha walifanikiwa kumkamata huku ikielezwa kuwa katika kijiji cha Makame ambako mara kwa wamekuwa wakikamata wawindaji haramu wa wanyama pori.

Nao baadhi ya wananchni Wilayani Kiteto wameitaka serikali kuboresha mawasiliano ya simu na barabara ili kurahisisha kutokomeza vitendo vya ujangili na kufikia adhima ya serikali kufanya hivyo.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.