MTANGAZAJI

NAIROBI:THE LIGHTBEARERS WAREKODI NYIMBO KATIKA STUDIO ZA HOPE CHANNEL AFRICA

Jumla ya Waimbaji 19 wa The LightBearers wako jijini Nairobi,Kenya  kwa ziara maalum ya uimbaji ambapo watashiriki kwenye Tamasha la Uimbaji litalofanyika kesho jumapili Agosti 30,mwaka kuanzia saa  8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni kwenye ukumbi wa Nairobi Cinema.

Leo Agosti 29 jioni walikuwa katika studio za Hope Channel Africa zilizopo yalipo Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) eneo la Ongata Rongai  ambapo wamerekodi nyimbo tano za video ambazo zitarushwa na kituo hicho cha Televisheni kinachorusha matangazo yake kupitia satalaiti kwa kushirikiana na Hope Channel International.

Baada ya Tamasha la kesho The LightBearers wataelekea jijini Arusha kisha Mwanza ambako watashiriki kwenye tamasha litakaloambatana na kuitambulisha album yao namba 3 iitwayo MUNGU kimbilio tukio litakalofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Mlango Mmoja Septemba 5 mwaka huu saa nane mchana.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.