MTANGAZAJI

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI TANZANIA ZIMEANZA RASMI

Mgombea wa CCM Dkt John Pombe Magufuli

Edward Lowassa

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania zimeanza rasmi juzi,ambapo Oktoba 25  mwaka huu wananchi watapiga kura kuchagua madiwani, wabunge na Rais


 Uzinduzi wa kampeni za Chama tawala CCM  umefanyika Agosti 23 mwaka huu katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam Dkt. John Pombe Magufuli  akigombea kupitia  chama hicho, huku ule wa  Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa ukitarajiwa kufanyika Agosti 29 mwaka huu.

Hata hivyo wakati kampeni hizi zikiianza nchini humo hisia za watanzania na wengi wanaofuatilia uchaguzi wa mwaka huu ambapo kuna wagombea wanane ziko kwa wagombea wa uraisi wawili John Pombe Magufuli ambaye aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali na Edward Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania jumla ya watanzania milioni 23 wamejiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa mfumo wa Biometric Voter Registration (BVR).BVR ni mfumo wa utambuzi wa wapigakura wengi na kwa haraka kwa kutumia alama za kibailojia kama vidole, macho au sauti.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.