RAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHAMMED SHEIN ALIPOKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI
Aliyesimama ni mwenyekiti wa umoja wa Tanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo akimkaribisha Rais Dr.Shein |
Balozi wa Tanzania nchi ujerumani Bw.Philip Marmo akimwagia sifa za watanzania ujerumani Rais Dr.Shein |
Rais wa Zanzibar Dr.Shein akiwa na watanzania Ujerumani |
Rais wa
Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dr. Ali Mohammed
Shein ameongea na watanzania katika mkutano na Diaspora uliofanyika
Würzburg nchini Ujerumani. Mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa
Watanzania Ujerumani UTU e.V, ulifanyika katika Hotel ya Maritim Hotel
mjini humo hivi karibuni.
Akianza kwa kufungua mkutano huo
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Bw. Philip Marmo
,alisema, watanzania wanaoishi Ujerumani wanaishi bila ya kuvunja sheria
nchini humo, na wanampa Mhe Balozi Marmo faraja kubwa kwani hajawahi
kusikia Mtanzania yoyote Aliye Jela au Aliye na kesi ya aina yoyote ile
tangu afike Ujerumani, taarifa alizonazo ni kwamba kila mtanzania
anafanya shughuli zake za kujitafutia riziki iliyo halali.
Bw. Marmo
alimpongeza sana mwenyekiti wa umoja wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo
Peter Mfundo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuendesha Umoja huo na
kuwasiliana na Ofisi ya Ubalozi mara mtanzania anapopatwa na shida ya
aina yoyote ile.
Naye mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani U T U
e.V Alieleza kwa ufupi madhumuni ya kuanzishwa Umoja huo ambayo kwanza
ni kukusanya watanzania na kuwa pamoja na kusaidiana katika shida kwani
miaka ya nyuma watanzania walikuwa wakipata shida nyingi laiki kwa vile
hapakuwa na chombo kinachowaunganisha ilikuwa ni tabu kujua nani na ana
shida gani, aidha alieleza kuwa UTU e.V ni chombo ambacho kitakuja
kuwajenga watoto wa kitanzania ambao wanazaliwa Ujerumani katika kujua
wapi walipotokea na wana fursa zipi ndani ya Tanzania.
Alifafanua
kwamba watanzania waliokwenda ujerumani wakiwa watu wazima wanajua nini
cha kufanya ili kupata fursa zilizopo Tanzania lakini watoto
waliozaliwa ujerumani labda watakosa mawasiliano na ndugu zao waliopo
Tanzania hivyo Umoja wa Watanzania Ujerumani kitakuwa ndio chombo chao
kitakachowaunganisha baina yao.
Naye
Mhe Rais wa Zanzibar Bw Ali Mohammed Shein alimalizia Hotuba yake kwa
kuwaasa watanzania wanaoishi Ujerumani wakae kwa amani na waendelee na
shughuli zao za kujitafutia riziki ya halali, aidha alisema Serikali ya
tanzania inapata faraja kubwa kuona Watanzania wanaishi nje ya nchi bila
ya kupamatatizo wala kusababisha matatizo, aliwaasa Watanzania
kuheshimu sehemu zao za kazi, ajira zao na kuzinyenyekea kwani sehemu
mtu anayopata riziki inapaswa inyenyekewe na kuheshimiwa,.
Kabla ya kufunga mkutano huo uliohudhuriwa na Watanzania wanaoishi ujerumani kutoka miji mbali mbali nchini humo,Mheshimiwa Rais Wa Zanzibar aliwaambia watanzania wasifikirie kuwekeza Tanzania bara peke yake kwani hata Zanzibar ni kwao hivyo wanakaribishwa wakati wowote
Kabla ya kufunga mkutano huo uliohudhuriwa na Watanzania wanaoishi ujerumani kutoka miji mbali mbali nchini humo,Mheshimiwa Rais Wa Zanzibar aliwaambia watanzania wasifikirie kuwekeza Tanzania bara peke yake kwani hata Zanzibar ni kwao hivyo wanakaribishwa wakati wowote
Post a Comment