MTANGAZAJI

AJALI YA AMBASSADORS OF CHRIST

Mdau Emanuel Sayo aliyeko Kahama ameifahamisha blog hii kuwa Waimbaji wa Ambassadors Of Christ toka Rwanda waliofariki ni Gatare Jim Ephrahim,Manzi Philibert na Amosi Phares.

Majeruhi ni Butera John Baptiste,Mutamba Patience,Grace Kavara,Mark Ndizeye na Sande Ndiramiye.
Kutoka kulia ni wawili Marehemu Gatare Jim Ephrahim mmoja wa waanzilishi na Amosi Phares (katikati mweye tshirt nyeusi) mmoja wa waimbaji wa Ambassadors of Christ na mtanzania pekee aliyekuwa akiimba kwaya hiyo na ndiye aliyekuwa akitafsiri nyimbo zao toka Kinyarwanda kuja lugha ya kiswahili hapa ilikuwa ni ndani ya studio namba 3 za Morning Star Radio katika mahojiano siku ya jumamosi iliyopita.

 Waimbaji watatu  wa Ambassadors Of Christ waliofariki ni waliofuatana kwa kusimama mstari wa nyuma kuanzia kushoto ni Gatare Jim Ephrahim,Manzi Philbert na Amos Phares

25 comments

salasala said...

Inahuzunisha sana, Mungu awafariji Ambassadors na familia zao. Maisha ya mwanadamu nikama maua.

mwendokasi said...

mh kweli hakuna ajuaye ya kesho. Leo ndio yako/yangu.

Anonymous said...

Maduhu inasikitisha sana ukiwa unasikiliza hizi nyimbo na kugua kuwa miongoni mwao wamelala lol, maduhu weka maelezo kwa zile picha ambazo hazina maelezo

Filipo Lubua said...

Mungu yuana mipango ambayo kwetu ni fumbo kuu. Ni kweli kama walivyoimba Muungano Christian Choir, tunatembea lakini sisi ni marehemu.

Beckie Kasika said...

Jamani am speechless, Mbona Mungu ameruhusu na hili litokee??? Am hurt. Mungu atusaidie na awafariji Ambassadors of Christ Amen

Anonymous said...

Jamani kifo hakina huruma...... Ningekuwa na uwezo wa kutia sahihi wanaofikwa na kifo, ningekataa kutia cheti cha waimbaji hao wapendwa. Tuliwapenda na tuna imani ya kuonana siku moja karamuni huko mbinguni. Pole kwa jamaa na marafiki.

Pr. Haruni N.E Kikiwa said...

Wapendwa jambo hili linasikitisha sana, hebu katika kipindi hiki kigumu Tumuombe Mungu atusaidiye kuzihesabu siku zetu. Poleni Ambassadors, ndugu na jamaa wawa fiwa Pamoja na wapenzi wa Music wa Kikristo wote Duniani.

Ombeni said...

Jamani ni masikitiko makubwa katika familia ya Bwana nimekuwa nikiwasikiliza waimbaji hawa lately. Tunawaombea faraja itokayou kwa Yesu katika kipindi hiki kigumu. It is such a loss nawaombea wazidi kuwa na imani wasikate tamaa. Shetani ameona anashindwa kufanya kazi yake hivyo kazeni mwendo ndugu zangu.

Unknown said...

Kifo sio ugonjwa, hakina hodi chaja pasipo hodi.. hakina huruma. Nawapa pole ndugu na jamaa kwa msiba mkubwa huu wa ghafla. Jina la bwana Yesu liimidiwe.

Anonymous said...

Poleni sana Christ AmbassadorMungu na awatie nguvu na majeruhi wapone haraka. Ama kwa hakika hata maneno ya kuandika yamenikosa. Ni habari ya kisikitisha sana jamani Kifo hakizoeleki. Gideon Kasozi alipotunga wimbo wa kifo hakukosea kweli kifo hakina hodi wala kinga wala hakuna dawa ya kukizuia na kikifika hakirudi nyuma. Na kila nafsi itaonja mauti wenzetu wametangulia nasi tupo nyuma tunawafuatakinachotakiwa tu nikujiweka tayari wakati wote maana hatujui wakati wala muda kifo kitakapo tufika. Amen

Victory Gospel Singers- Arusha said...

Hakika maisha ya mwanadam ni maua. Tumeshtushwa sana na ajali na msiba wa marafiki zatu AMBASSADORS OF CHRIST, tunawapenda sana, jipeni moyo wala msikate tamaa haya ni majaribu ya ibilisi. Majeruhi wote tunawaombea uponyaji toka kwa Mungu. Ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa Ambassadors pote duniani Bwana awape faraja ya pekee! maana INAUMA!!

Unknown said...

Kweli ni habari ya kusikitisha sana jamani kuondokewa na wapendwa wetu mungu awalaze pema. na wape faraja wafiwa wote!!!!

Anonymous said...

This is more than sad.

Anonymous said...

Ni hakika Mungu alituficha kitu kikubwa sana, laiti kama kila mtu angejua siku ya kufa kwake, angejiweka tayari na kumsubiri Bwana. Lakini hakuna ajuaye siku wala saa. Poleni sana ndugu zangu mliofikwa na msiba, Mungu aishie milele yu pamoja nanyi. Poleni sana Ambassadors na ndugu wengine.

samson Poneja said...

Tuwaombee majeruhi wapate nafuu na kuendelea na wito wao wa kueneza injili yao kwa njia ya nyimbo. Nashauri wale walioandaa tamasha na mwaliko huu waandae safari ya kuelekea huko kwa ajili ya kusalimia majeruhi na familia zilizofiwa na ingekuwa vema hili litangazwe katika makanisa na gharama ni kiasi gani ili wanaoweza waende

Elias said...

Kaka Maduhu, Wazo la Samsoni Poneja hapo chini ni zuri na la maana sana. Kwa kushirikiana na Accacia hebu ratibuni wazo hili vizuri. Nitakuwa mmja wao. Ubarikiwe mtumishi.

Anonymous said...

nilishindwa kuelewa na kuamini nilipoiona taarifa ya ajali ya watumishi wa Mungu Ambassadors of Christ, shetani ana njia nyingi za kutudhoofisha lakini hakika mwisho wake uko karibu,hakika huzuni zetu zitakuwa furaha siku hiyo inakuja.

Anonymous said...

Inasikitisha sana lakini yote Mungu anayajua,Mungu awabariki sana na mzidi kuifanya kazi yake katika jina la Yesu Kristo.

Jeremiah Msigwa said...

Too soon jamani!!!!!
Shocking news dah,may God provide all conmfort from His throne!

THE GOLDEN CROWN, ARUSHA UNIVERSITY said...

RATIBA YA MUNGU HAIJULIKANI KWETU CHA MUHIMU TUJIWEKE TAYARI ILI YESU AKIJA TUMLAKI, HUKO TUTAKUA NA WAPENDWA HAWA TENA, NA CHA KUFURAHISHA NI KUA TUTAIMBA KWAYA PAMOJA NAO, TUSITISHIKE NA HILA ZA SHETANI KWAKUA MARAZOTE SHETANI HANA UBAVU WA KUMWANGUSHA MTUMISHI WA BABA.

Anonymous said...

Bado nasikitika kwani utadhani ni watu ninaowafaham.

MAKYAO said...

KWAKWELI KIFO CHA MWANADAMU NI FUMBO KUBWA.ILA MUNGU ANABAKIA KUWA MUNGU HATA KAMA SISI WANADAMU HATUNA MAJIBU SAHIHI KWA NINI VIFO KAMA HIVI VIMETOKEA.

ZAWADI MAKYAO said...

THOUGH I FELT SO SORRY WHEN I GOT THESE SAD NEWS, GOD REMAIN FAITHFUL.

FARAJA MAKYAO said...

MAY THE ALMIGHY GOD BE WITH THE REMAINED GROUP OF AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR IN THIS TIME OF SORROW.

MARTHA MAKYAO said...

TUKIO HILI NI HUZUNI KUBWA KWETU WANADAMU.NI MUNGU TU AWEZAYE KUTUFARIJI.

Mtazamo News . Powered by Blogger.