ARUSHA:MTANZANIA ASHINDA TUZO YA UBUNIFU NA KUZAWADIWA SHILINGI MILIONI 77
Dr Askwar Hilonga (kulia) akipokea tuzo. |
Dr Askwar Hilonga akionesha jinsi vichujio vya maji vinavyofanya kazi huko Karatu,Tanzania (Picha zote na BBC) |
Mshindi wa Tuzo ya Ubunifu iliyotolewa na taasisi ya Uingereza ya uhandisi ya Royal Academy of Engineering Mtanzania Dr Askwar Hilonga amesema kiasi cha dola 38,000 za kimarekani sawa na shilingi milioni 77 za kitanzania alizotunukiwa atazitumia katika kuendeleza mradi wake wa kusafisha maji hasa katika maeneo ya vijijini.
Akizungumza hii leo baada ya kuwasili
toka nchini Afrika ya Kusini Dr Hilonga ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu
cha Afrika cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichopo jijini Arusha
amesema kupata tuzo hiyo kutaweza kukuza biashara yake kwa kasi kwani lengo ni kuwafikia watanzania
wengi mapema iwezekanavyo ili kutokomeza
magonjwa ya tumbo, kuharisha, Amoeba,madhara ya Fluoride kwenye meno na mifupa
kunakosababishwa na maji yasiyo salama.
Dr Askwar Hilonga,aliyeshindanishwa na washiriki 55 toka nchi
15 za bara la Afrika ametengeneza chujio maalum ya maji ambayo inatumia
mchanganyiko wa mchanga na teknolojia ya nano inayotumika kuua wadudu na
kuondoa chemikali zilizoko kwenye maji.
Kwa sasa teknolojia hiyo imeshaanza kutumika katika maeneo ya
wilaya ya Arumeru na Karatu huku
ikitarajiwa kuwasaidia watu wengi barani Afrika wanaosumbuliwa na magonjwa ya tumbo na hasa watoto chini ya umri
wa miaka mitano.
Post a Comment