MTANGAZAJI

ARUSHA:NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA AKITAKA CHUO KIKUU CHA ARUSHA KUFANYA MAHUSIANO NA VYUO VIKUU VYA NJE

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari,Vijana,Utamaduni na michezo Prof.Elisante Ole Gabriel (wa tatu toka kulia) makundi yaliyopewa medali pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Arusha.
 Meneja Uzalishaji wa Morning Star Televisheni Daniel Bulengela akitoa maelezo kwa Prof.Elisante Ole Gabriel.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya habari,Vijana,Utamaduni na michezo Prof.Elisante Ole Gabriel ameishauri bodi ya Chuo kikuu cha Arusha kufanya mahusiano ya karibu na vyuo vya nje ya nchi ili kuongeza ufanisi katika taaluma hasa katika kubuni na kugundua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Prof Elisante aliyasema haya Jana may 26,2015 alipokuwa akifungua maonyesho ya pili ya bidhaa mbalimbali za ubunifu kwa wanafunzi katika chuo Kikuu cha Arusha .

Ambapo makundi mbalimbali yalipata medali za ufaulu katika ubunifu na ugunduzi baada ya kutembelea mabanda mbalimbali likiwemo banda la Morning star Televisheni.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.