MTANGAZAJI

TABORA:ASKARI POLISI AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI



Polisi aliyefahamika kwa jina la Charles mwenye nambari H 3416 wa Kituo cha Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, amejiua kwa kujipiga risasi akiwa ndani ya kituo hicho tukio hilo lilitokea siku ya jumamosi na imeelezwa sababu za kujiua kwake hazijafahamika.

Wakizungumza na vyombo vya habari baadhi ya wananchi walio jirani na kituo hicho, wamesema tukio hilo lilitokea saa moja jioni ambapo wananchi hao wamesema, kutokana na hali hiyo walilazimika kuwauliza baadhi ya askari waliokuwa naye zamu, ambao nao walidai hawajui sababu za mwenzao kuchukua uamuzi huo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda amesema  ni kweli askari huyo amejiua wakati akiwa kituoni saa moja usiku, na uchunguzi unaendelea kujua sababu za kifo chake.

Kamanda Kaganda amesema askari huyo hakuacha ujumbe wowote kueleza sababu za kujiua kwake. 





No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.