DAR ES SALAAM:HATIMAYE TUZO YA JAMII 2015 YATOA TUZO SABA ZA JAMII
Wawakilishi wa waliopewa tuzo katika picha ya pamoja na mgeni rasmi |
Mwenyekiti wa Kampuni ya Tanzania Awards International LTD Ndugu DJ Malegesi akitoa maelezo ya Tuzo ya Jamii 2015 |
Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymondi Mushi akihutubia |
Katibu wa Tanzania Awards International LTD Amani Mwaipaja akitoa maelezo ya tuzo |
Mkurugenzi wa Push Mobile Fredy Manento |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa kitukuu wa Hayati Julius Kambarage Nyerere |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akikabidhi Tuzo ya Heshima ya Nelson Mandela kwa Kiongozi wa Mtandao wa Vijana Tanzania |
Mwakilishi wa Familia ya Makamba (Kulia) akipokea Tuzo ya Mwanasiasa kijana aliyopewa January Makamba |
Mwakilishi toka Chama cha Wananchi -CUF(kulia)akipokea tuzo kwa niaba ya Tume ya haki za binadamu na utawala bora |
Angel Magoti akiimba wimbo maalum |
Kikundi cha Sanaa cha Tuzo ya Jamii 2015 kilitumbuiza |
Viongozi wa Watu wenye albinism wakiwa katika picha na Mgeni Rasmi pamoja na viongozi wa Tanzania Awards Intenational LTD |
Kampuni ya Tanzania Awards International Limited ya jijini Dar es salaam imetoa Tuzo saba za Jamii zikiongozwa na tuzo ya Heshima kwa Rais wa awamu ya kwanza wa Tanzania Hayati Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini hayati Nelson Mandela kwa juhudi na uzalendo waliofanya kipindi cha uongozi wao.
Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Jamii iliyofanyika Aprili 13,mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymondi Mushi ameipongeza Kampuni hiyo kwa kutoa tuzo hizo katika Jamii na kusema kuwa zinachochea uongozi bora katika Jamii na uwajibikaji.
Mushi Amesema kila mwananchi anapaswa kuwa kiongozi bora kwa mwenzake ili kuiga mifano ya viongozi hao wa zamani ambao waliitumikia nchi na kuacha historia ambazo mpaka leo zinawakumbusha viongozi kutumikia nchi na kuwa wazalendo.
Licha ya tuzo mbili zilizo kwenda kwa waasisi wa Taifa la Tanzania na Afrika ya Kusini,tuzo nyingine imetolewa kwa Dkt Regnald Mengi kama mtu mwenye mchango mkubwa kwa Jamii,Ndugu Otieno Igogo mlipa kodi bora,Tume ya haki za binadamu na utawala bora,January Makamba mwanasiasa kijana na Mwanasiasa Mtu mzima kwa Profesa Sospiter Muhongo waziri mstaafu wa Wizara ya nishati na madini.
Post a Comment