MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:TUZO ZA GLORIOUS MUSIC AWARDS 2015 ZA MORNING STAR TV ZAFIKA KATIKA JUMA LA PILI


Neema Charles mwimbaji wa Kwaya ya PF Kitunda Kati
 

Baadhi ya Waimbaji wa Family Music
Kikundi cha Inzamba

Uwanjani SDA Choir wakiimba 
 Mchakato wa kuwapata waimbaji watakaopata Tuzo za Glorious Music Awards 2015 zitakazotolewa na Morning Star Televisheni umefikia wiki ya pili baada ya jana kufanyika kwa mara ya pili toka mchakato huo ulioanza Aprili 12,mwaka huu.

Miongoni mwa vipengele vilivyopo katika tuzo hizo ni Kikundi cha Mwaka,Kikundi Bora,Waimbaji Bora,Mtunzi Mahiri,Mpangaji Muziki Mahiri,Kwaya ya Watoto,Mwanamuziki wa Kiume Mahiri,Mwanamuziki wa Kike Mahiri,Mwanamuziki wa Kike anayeibukia,Mwanamuziki wa Kiume anayeibukia na Kikundi Kinachoibukia.

Mchakato wa kuwapata waimbaji watakaopata tuzo hiyo ambayo kwa mwaka huu itatolewa kwa waimbaji Waadventista Wa Sabato walioko jijini Dar es salaam unaoneshwa na Morning Star Tv jumapili saa 2:00 usiku na jumatatu saa 1:00 jioni.(Picha zote na Emanuel Feruzi wa www.k15.photos)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.