MTANGAZAJI

MKUTANO WA KUIGAWA KONFERENSI YA MASHARIKI MWA TANZANIA YA WAADVENTISTA WASABATO KUFUNGULIWA KESHO


Mkutano mkuu wa tatu wa kuigawa Konferensi ya Mashariki mwa Tanzania ya kanisa la Waadventista Wa Sabato (ETC) unaratajiwa kufunguliwa kesho mjini Morogoro.


Tukio hilo ambalo litakuwa ni kwa ajili ya kupanga  konferensi mbili mpya litatanguliwa na kuvunjwa rasmi kwa konferensi ya mashariki ,zoezi litakalo simamiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Kanda ya Afrika Mashariki na Kati Dr Nathaniel Walemba.


Konferensi zinazotarajiwa kupangwa ni Konferensi ya Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC) na Konferensi ya Mashariki na Kati mwa Tanzania (ECT).


Akiongea na Morning Star Radio hii leo Katibu Mkuu wa ETC Mchungaji Sadock Butoke amesema konferensi hiyo ina makanisa 305 ambalo ni ongezeko la asilimia 26 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita,mitaa 81,makundi 373 na jumla ya washiriki 67,928


Mchungaji Butoke ameyataka makanisa mahalia yote kuwa na makundi kwa uchache kila kanisa liwe na makundi yasiyopungua matatu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.