MTANGAZAJI

MAMBO YANAYOTARAJIWA KUJIRI MWAKA 2015 NCHINI TANZANIA

 
Januari: Uandikishaji wapiga kura- Mwishoni mwa mwezi huu uandikishaji upya wa wapigakura utaanza nchi nzima, mchakato ambao utasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Februari: Uamuzi mgumu CCM- Chama cha Mapinduzi (CCM), kiitatoa uamuzi kuhusu wanachama wake waliotiwa hatiani kwa kufanya kampeni mapema na vitendo vilivyokiuka maadili ndani ya chama na ndani ya jamii.

Machi: BRT kukamilika- Mradi wa ujenzi wa barabara ya mabasi ya endayo haraka (BRT) kuanzia Kimara hadi Posta na Moroco-Magomeni utakamilika chini ya Mkandarasi Strabag International kutoka Ujerumani na Mhandisi Msimamizi SMEC International ya Australia.

Aprili: Kura za maoni- Aprili 30 itakuwa ndiyo siku ya upigaji wa kura za maoni za ama kupitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mei: CCM vs Ukawa- Vyama vya siasa vinatarajiwa kuanza kuteua wagombea wa nafasi za urais na hapa ndipo mchuano kamili kati ya CCM na Ukawa unatarajiwa kuanza rasmi.

Juni: Bajeti ya kwanza- Mkutano wa Bunge la Bajeti utapitisha Bajeti ambayo sehemu yake itatumiwa na Serikali ya awamu ya tano, hivyo itatoa taswira ya uchumi wa Serikali ijayo chini ya rais mpya baada ya Jakaya Kikwete kumaliza ngwe yake

Julai: Bunge kuvunjwa- Mkutano wa 20 wa Bunge utakamilika na Bunge litavunjwa na Rais Kikwete, ikiwa ni ishara ya kupuliza kipenga cha wabunge na wananchi wengine kuanza mbio kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Agosti: Kampeni kuanza-Ni mwezi ambao zitaanza rasmi kampeni za uchaguzi mkuu, kwa vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu kuaomba ridhaa ya wananchi kwa kunadi sera zao ili vipate fursa ya kuwaongoza.

Septemba: Ligi Kuu Bara- Msimu mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utaanza ambapo timu kadhaa zitashiriki ligi hiyo inayaotarajiwa kuwa na mikikimikiki , ligi inayoendelea ilikuwa imejaa matukio mengi yakiwamo ya kufukuza makocha.

Oktoba: Rais Mpya- Utafanyika Uchaguzi Mkuu wa kumpata rais mpya atakayeongoza Tanzania hadi 2010. Vyama zaidi ya 20 vya siasa vinatarajia kusimamisha wagombea katika nafasi mbalimbali.

Novemba: Rais kuapishwa- Matokeo ya uchaguzi Mkuu yatakamilika na Jaji Mkuu atamwapisha Rais mpya kushika madaraka hayo ya juu nchini. Shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika mbele ya viongozi mbalimbali maarufu wa ndani na nje ya nchi. Baada ya hatua hiyo Rais Kikwete ataingia rasmi kwenye orodha ya marais wastaafu.

Desemba: Sherehe za uhuru- Rais mpya atapata fursa ya kukagua gwaride la kwanza la miaka 54 ya Uhuru, ikiwa ndio sherehe yake ya kwanza ya kitaifa tangu kuapishwa kwake.

CHANZO:Mwananchi Communication LTD

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.