MTANGAZAJI

PICHA:SABATO YA SHUKRANI ILIVYOKUWA KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO MANZESE JANUARI 3,2015






Mchungaji Stephen Letta  akihutubia

Mchungaji David Mmbaga na Mch Stephen Letta

Mbiu Kwaya toka Tandale ikiimba



Kwaya ya Sauti ya Nyikani toka Sinza ikiimba



Mass Choir inayoundwa na waimbaji wa kwaya za Mbiu,Angaza na Sauti ya Nyikani







Mwalimu Joseph Ligala wa Mbiu Kwaya






Waumini wakitoa sadaka ya shukrani ambayo itasaidia kuwasomesha wachungaji



Chakula kilikuwepo kwa watu wote


Kanisa la Waadventista Wa Sabato mtaa wa Manzese unaojumuisha makanisa matatu Tandale,Sinza na Manzese chini ya Mchungaji David Azaeli Mmbaga yalifanya mkutano wa sabato ya shukrani ya kumaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka mpya wa 2015.

Mkutano huo uliofanyika katika kanisa la Manzese siku ya sabato ya kwanza ya mwaka 2015 mbali na kuhudhuriwa na waumini wa makanisa hayo uliambatana na ibada,maombi na nyimbo toka kwa waimbaji wa kwaya tatu za mtaa huo ambazo ni Mbiu,Angaza na Sauti ya Nyikani ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa Chama cha Wachungaji wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato Mch Stephen Letta.

Mwishoni mwa ibada waumini walitoa sadaka za shukrani ambazo zitasaidia kuwasomesha wanafunzi wa uchungaji katika Chuo Kikuu cha Bugema kilichopo nchini Uganda,ibada ya ilipomalizika watu waliohudhuria walishiriki kwa chakula cha mchana huku wachungaji na wazee wa kanisa wakihudumia kugawa chakula kwa mamia ya waumini waliokuwepo na baadaye mchana kulikuwa na uimbaji toka kwa waimbaji mbalimbali.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.