IRINGA:305 WABAINIKA NA VVU BAADA YA KUPIMA KWA HIARI
Watu
wapatao 305 kati ya watu 4,879 mkoani Iringa waliopima afya zao kwa hiari katika kipindi cha robo ya
kwanza ya Mwaka huu wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
Akizungumza
katika kikao cha utekelezaji wa shughuli za Ukimwi Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudhibiti Ukimwi ambaye pia ni
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, ametoa taarifa zilizotekelezwa
na Kamati hiyo mbele ya Baraza la Madiwani.
Ndaki amesema kuwa kati ya waliojitokeza
kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa 2,417 na wanawake 2,467
ambapo kati ya watu 305 waliopima
kwa hiari na kukutwa na maambukizi, wanaume walikuwa 124 na wanawake 181.
Naibu
meya huyo amedai kuwa huduma ya
kuzuia maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto imezingatiwa
huku, wajawazito 1,036 wakijitokeza na kupata ushauri nasaha na kupima wakati
ambapo kati yao wajawazito 10 sawa na asilimia moja walikutwa na maambukizi.
Post a Comment