MTANGAZAJI

WAZIRI MKUU ATAKA VITA DHIDI YA UJANGILI IWE YA PAMOJAIMG_5158
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri mara  baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga Mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Waziri wa Mali asili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu na wa pili kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu


IMG_5167
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli kwenye chumba maalum cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufunga mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanyamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014.

IMG_5170
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, huku Waziri wa Mali asili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akifurahi jambo ndani ya chumba cha mapumziko kabla ya kuelekea kwenye chumba cha mikutano.
IMG_5169
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli (wa pili kulia) kwenye chumba cha mapumziko baada ya kuwasili ukumbi hapo. Kushoto ni  Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu.
IMG_5182
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, kwenye chumba maalum cha mapumziko.
IMG_5253
Waziri wa Mali asili na utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kushoto) kufunga rasmi mkutano wa kupiga vita dhidi ujangili wa wanayamapori  na kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magese Mulongo, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli wakiwa meza kuu.

Waziri Mkuu wa Tanzania   Mizengo  Kayanza Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma  mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha,Waziri Mkuu amesema suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika, taasisi, wananchi na viongozi wote kama wadau wakuu. 

Ili kutekeleza azimio hilo, ameshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake,timu ambayo itakutana  kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji wake.

Pia amesema waandishi wa habari nao wanasehemu ya kufanya  katika kukabiliana na tatizo la ujangili nchini ambapo serikali inatafuta mpango wa kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.