WAADVENTISTA WA SABATO KUAMUA KAMA WATAWAWEKEA MIKONO YA KICHUNGAJI WANAWAKE JULAI MWAKANI
Kanisa la la Waadventista Wa Sabato ulimwenguni huenda likaamua kama litapitisha huduma ya
kuwawekea mikono ya kichungaji wanawake na kuwatenga rasmi kwa kazi hiyo
kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Kanisa hilo Julai
mwakani.
Uamuzi huo
umetolewa mapema juma hili na halmashauri kuu ya kikao cha mwaka cha kanisa la Waadventista wa Sabato
duniani kilichofanyika yalipo makao makuu ya kanisa hilo nchini Marekani ambapo kura 243 kati ya kura 287
ziliunga mkono kusitisha suala hilo mpaka kikao cha mwaka 2015
Kumbukumbu za
kanisa hilo zinaonesha kuwa suala la kuwawekea mikono ya wanawake limeanza
kujadiliwa miaka 130 iliyopita lakini miaka ya sabini ndipo lilipoanza kupamba
moto na hasa katika maeneo ambako washiriki wanataka mabadiliko ikiwemo
Marekani baadhi ya maeneo ya Ulaya na kusini mwa Pasifiki huku kamati kuu ya
uchaguzi ya kanisa hilo ya mwaka 1990 na 1995 ilipendekeza suala hilo na ajenda
hiyo haikuwahi kujadiliwa toka wakati huo.
Mkutano wa
Halmashauri kuu ya kanisa la waadventista wasabato hufanyika kila baada ya
miaka mitano ambapo hukutanisha zaidi ya viongozi 338 wa ngazi za juu za kanisa
kutoka divisheni 13 ulimwenguni ,Takribani miaka 2 imepita toka wajumbe
kupatiwa muda wa kutafakari kuhusu wanawake kuwawekea mikono ya kichungaji
ambapo Oktoba 14 mwakani swala hilo linatarajiwa kuamuliwa kwa kupigiwa kura.
Post a Comment