MTANGAZAJI

MCHUNGAJI ALIYETEKWA AACHIWA HURUMchungaji Sergei Litovchenko
 
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Horlivka, Sergei Litovchenko lilipo mashariki mwa Ukraine ameachiwa huru na kurejea katika familia yake baada ya kutekwa na watu wasiojulikana kwa takribani siku 20.

Msemaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Horlvka, Garrett Caldwell amesema kuwa wamefurahi kufahamu kuwa Mchungaji yuko huru akiwa na afyan njema na amewashukuru wale wote walioshiriki katika kumuombea Mchungaji huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa mwanaume ambae hakuweza kutambulika aliingia katika kanisa dogo la Waadventista Wa Sabato  wakati wa ibada ya meza ya bwana ambapo aliwalazimisha waumini kutawanyika na kumlazimisha mchungaji kuingia kwenye gari na kutokomea nae kusikojulikana. 
Mchungaji Sergei Litovchenko alitekwa tarehe 27 septemba mwaka huu na mwanaume aliyevalia mavazi ya kuficha uso na kurejea katika familia yake jana tarehe 16 oktoba mwaka huu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.