ABOUD JUMBE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI
Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud
Jumbe Mwinyi (94), amelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
Akizungumza na wanahabari hii leo Ofisa Uhusiano wa
Hospitali ya Muhimbili, Doris Ishenga,amesema Jumbe alipokewa
hospitalini hapo tangu Oktoba 12, mwaka huu na amelazwa katika Taasisi ya
Moyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Amsema kwa mujibu wa taarifa
za madaktari za Kitengo cha Moyo hospitalini hapo, baada ya kumfanyia
uchunguzi wamebaini Jumbe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo hali
inayobabishwa na kuwa na umri mkubwa.
“Ni kweli Alhaj Jumbe alifikishwa
hapa Muhimbili tangu Jumamosi iliyopita na amelazwa katika wodi ya moyo
akisumbuliwa na maradhi ya moyo.
“Unajua ugonjwa huu unawapata zaidi
watu wenye umri mkubwa, madaktari wamesema hali yake si mbaya na wala si
nzuri sana,” alisema.
Jumbe alikuwa Rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972
hadi 1984 akishika nafasi hiyo baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa
Kwanza wa Zanzibar, marehemu Abeid Aman Karume Septemba 5, 1972.
Alijiuzulu mwaka 1984
nafasi hiyo ilichukuliwa na Ali Hassan Mwinyi mwaka 1984, ambaye
baada ya mwaka mmoja alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Post a Comment