MTANGAZAJI

RIPOTI YA WHO:TANZANIA KATIKA NAFASI YA PILI BARANI AFRIKA KWA IDADI YA WATU WANAOJIUA


 

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetowa ripoti yake inayosema kwamba idadi ya watu wanaojiua duniani imeongezeka na kufikia kiwango cha kutisha.

 Ripoti inasema kwamba katika kila sekunde 40 mtu mmoja anajiua.Shirika hilo limelitaja tatizo hilo kama la kiafya ambalo linahitaji kushughulikiwa baada ya kufanya utafiti wake katika nchi 172 duniani.Barani Afrika nchi zilizotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojiua ni Msumbiji,Tanzania,Burundi Sudan Kusini na Uganda.

Tanzania iko katika nafasi ya pili barani Afrika ikiwa na asilimia 24.9 ya vifo hivyo vya kukusudia.Je tatizo ni nini? Saumu Mwasimba alimuuliza suali hilo mwanasaikolojia na Mchungaji Robert Mutangwa Ruiza kutoka Iringa Tanzania na alikuwa na haya ya kueleza.Sikiliza hapa http://www.dw.de/who-idadi-ya-watu-wanaojiua-duniani-yaongezeka/a-17903661

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.