MOROGOGO:MAGARI YATEKWA NA ABIRIA KUPORWA MALI
Watu wanaosadikiwa
kuwa ni majambazi wamefunga barabara ya Morogoro – Iringa katika eneo la njia
panda ya kilosa na kisha kuteka magari na kupora mali za abira.
Tukio hilo ambalo
lilitokea saa 8:30 usiku wa kuamkia jana, ikiwa ni siku moja baada ya polisi
mkoani humo kumtia mbaroni raia mmoja wa Burundi akiwa na vifaa mbali mbali
vinavyotumika katika utekaji wa magari.
Kwa mujibu wa baadhi
ya watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa watekaji walikua wakirusha mawe
na kuvunja vioo vya magari yaliyokuwa yamefika katika eneo hilo, kwa mujibu wa
dereva wa gari la kampuni ya MCL, Deo Ngangaa amesema kuwa walipofika eneo hilo
la tukio walisikia milio ya risasi na mawe yaliyokuwa yakirushwa.
Hata hivyo dereva
huyo amesema walipofika njia panda ya kilosa, kando ya barabara walioona magogo
na mawe huku magari matatu yakiwa yamepinduka, huku akisema wameshuhudia watu
kadhaa wakiwa wameanguka chini akiwemo dereva wa gari lililokuwa likipelekwa
Zambia ambaye pia ni raia wa nchi hiyo aliyejeruhiwa kwa kupigwa na mawe.
Post a Comment