MMOJA ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUJIFANYA MTUMISHI USALAMA WA TAIFA
Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutokana na makosa mbalimbali ya kujifanya ni
mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Mtu huyo anayejulikana kwa jina la GUNNER
SAIMON MEENA, Mkazi wa Kinyerezi Segerea, anatuhumiwa kuwasumbua
wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kuwasingizia au kuwatuhumu
kwamba wanahusika na makosa yenye kuhatarisha usalama.
Kwa muda mrefu Jeshi la Polisi limekuwa
likimtafuta mtu huyo kutokana na malalamiko mengi ambayo yamekuwa
yakijitokeza na uchunguzi unaonyesha kwamba jina lake halipo katika orodha ya
watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale
alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya kisomali aitwaye ABDI MOHAMED
DALMAR.
Mlalamikaji alitoa taarifa na ndipo mtuhumiwa akakamatwa katika mtego wa Polsi, Uchunguzi zaidi wa shauri hili unafanyika na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya jalada la kesi yake kupitiwa na mwanasheria wa Serikali.
Post a Comment