MTANGAZAJI

ARUSHA:WANANCHI WATISHIA KUCHOMA KIWANDA CHA VYANDARUA KWA SABABU YA UHARIBIFU WA MAZINGIRAZaidi ya wananchi 3000 katika kata ya Matevesi jijini
Arusha wameandamana na kutishia kuchoma moto kiwanda cha kutengeneza vyandarua cha A TO Z kinachomilikiwa na raia wa kiasia kilichopo Kisongo jijini Arusha,kutokana na madai ya kutiririsha maji machafu yenye kemikali na harufu kali yanayosababisha miguu  kubabuka namifugo yao kutozaa  takribani miaka mitatu.

Hali hiyo iliyotokea mwishoni mwa juma lililopita ililazimika askari polisi wenye silaha kufika eneo la tukio baada ya wananchi hao jamii ya wafugaji kuzingira majengo ya kiwanda wakiwa na silaha mbalimbali za jadi zikiwemo sime, na fimbo,  nakusababisha hali ya taharuki.

Kwa upande wa afisa mwajili wa  A To Z,Godwin Aberd amesema kuwa wameagiza mashine ambazo zitakuwa na uwezo wa kusafisha maji hayo pindi yanapotoka kiwandani ili yaweze kutumika tena kiwandani nakuahidi kutoyaruhusi kutoka nje.

Bw Abed amesema kuwa mashine hizo zimechelewa kufika nchini kutoka nje ya nchi,ila watafanya kila njia kuhakikisha zinachukua muda mfupi kuwafikia ili zianze kutumika mara moja kiwandani hapo na kuondoa changamoto hiyo.

Jeshi la polisi  wilayani humo kwa kushirikiana na uongozi wa jiji hilo walifanikisha kutuliza hasira za wananchi hao ambao walikuwa hawataki kutoka kiwandani hapo

Hata hivyo baada ya majadiliano ya muda mrefu kwa kuwatumia wazee wa jadi wa eneo hilo zoezi hilo lilifanikiwa kwa  sharti la kutoona maji yakiririka tena kwenye makazi yao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.