MARA:WAHUKUMIWA MIAKA MITATU KWA KOSA LA KUWATOROKA POLISI
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoani Mara imewahukumu
kwenda jela miaka mitatu kila mmoja watu wawili baada ya kukutwa na kosa la
kuwatoroka askari polisi wakiwa chini ya ulinzi.
Kabla ya huku hiyo kutolewa mahakamni hapo julai 3 mwaka
huu,mwendesha mashitaka wa serikali Fransisi Kyela aliiambia mahkama hiyo kuwa
juni 30 mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi watuhumiwa ambao ni Musa
Daniel(32)mkazi wa kijiji cha Buhemba wilaya ya Butiama,Machage Marwa (37)mkazi
wa kijiji cha Buhemba wilayani Butiama,Maribe Magori (34)mkazi wa kijiji cha
Buhemba na Chacha Mtatiro (28)mkazi
wawilaya ya Serengeti.
Watuhumiwa hao wakiwa ndani ya mahakama ya mkoa wakati
wakiwa wanakabiliwa na kesi za mauaji kabla ya mahaka kuanza watuhumiwa
walipitia dirishani kwa kuruka na kuanza kutimua mbio.
Mwendesha mashitaka wa seriklai aliiambia mhakama kuwa
wakati watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za kukimbia mtuhumiwa mmoja ambaye
alimtaja kwa jina la Machage Marwa alijeruhuliwa kwa kupigwa risasi mbili,sehemu
za kiunoni na mguu wa kushoto,hali iliyopelekea kupoteza uhai wakati wakatai
akipata matibabu katika hosptali ya mkoa mjini hapa.
Hakimu Richard Maganga aliyekuwa akisiliza kesi hiyo baada
ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na baadhi ya wananchi waliokuwepo
mahakamani siku ya tukio,mahakama ilitoa nafasi kwa mwendsha mashitaka wa
serikali kutoa pendekezo la aina ya adhabu kwa watuhumiwa.
Mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali
kwa watuhumiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kama hiyo ya
kutoroka wakiwa chini ya ulinzi.
Kufuatia ombo la mwendesha mashitaka mahakama hiyo
mewahukumu watuhumiwa hao kwenda jela miaka mitatu kila mmkoja huku wakiendelea
kukabiliwa kesi ya mauaji waliyokuwa nayo awali.
Post a Comment