TRL KUANZA USAFIRISHAJI WA ABIRIA RELI YA YA KATI JUNI 3,2014
Uongozi wa
kampuni ya reli Tanzania TRL nchini 
umetoa taarifa kwa wananchi na wateja wake wanaosafiri kwa kutumia
usafiri wa garimoshi  kwa reli ya kati  kuwa huduma ya usafiri itaanza tena juni 3
mwaka huu.
 Uamuzi 
huo unatokana na kukamilika kwa kazi ya ukarabati wa reli eneo la kati
ya stesheni ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma,baada ya eneo hilo
kuharibiwa vibaya na mafuriko ya mvua kubwa zilizonyesha kati ya mwezi January
hadi April mwaka huu.
Shirika hilo
pia linawashauri wateja wake na wananchi kwa ujumla kuzingatia utaratibu wa
safari na kuandaa mapema mizigo inayozidi uzito wa kawaida uliwekwa  na mamlaka husika ili ifanyiwe usajiri  mapema na kusafirishwa siku moja kabla ya
safari.
Meneja mkuu
wa TRL ndugu Lowrand Simkengu amesema  wananchi na abiria wote kwa ujumla  wanapaswa kuzingatia  muda wa kuondoka kwa garimoshi kwa siku ya
jumanne na ijumaa kutoka stesheni ya Dar kwenda Kigoma na Mwanza 
Simkengu
ameongeza kuwa muda wa kuondoka kwa gari moshi ni  saa 11 jioni  kwenda Mwanza na Kigoma, na Mwanza kuja Dar  es salaam siku ya alhamisi na jumapili  itakuwa saa 12 jioni.

Post a Comment