KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO TANZANIA LAFANYA MABADILIKO YA UONGOZI KWA BAADHI YA TAASIS
Kamati kuu ya Union ya Kusini ya kanisa la
waadventista wasabato nchini Tanzania , hivi karibuni imefanya mabadiliko ya
viongozi na watendaji wa taasisi za kanisa hilo.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo kwa wafanyakazi wa Morning
Star Radio na Morning Star Televisheni na Mshauri na mlezi wa Taasisi hizo Mchungaji Robson Nkoko kwa niaba ya Mwenyekiti
wa Kamati ya unioni Mchungaji Magulilo Mwakalonge ambaye
ndiye mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato katika Union hiyo, imemteua
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni hiyo Mchungaji Robson Nkoko kusimamia utendaji wa vyombo vya habari vya kanisa hilo.
Na aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa hilo,
Mchungaji Musa Mika ameitwa kufanya kazi ya kufasiri katika kiwanda cha
uchapishaji cha kanisa (TAP) kilichopo
mjini Morogoro.
Wakati huo huo aliyekuwa Mhazini wa Tanzania
Adventist Press Bwana Mathias Mavanza amechaguliwa kushika nafasi ya aliyekuwa Mhazini wa Taasisi ya Vyombo vya
Habari vya Kanisa la Waadventista Wa
Sabato Tanzania, Koheleth Manumbu, ambaye ameitwa kuwa Mhasibu wa Kitengo cha
Huduma ya Nyumbani, Elimu na Maisha Bora (HHES) kilichopo Morogoro.
Kanisa la Waadventista wasabato nchini Tanzania
inamiliki Morning Star Radio, Studio ya Redio ya Waadventista Ulimwenguni na
Morning Star TV iliyoko katika maandalizi ya kuanza matangazo.
Post a Comment