MOSHI:WAKAZI WAHOFIA KUWEPO KWA UGONJWA WA DENGUE
Hofu
imetanda kwa wakazi wa Manispaa ya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakihofia kuumwa na mbu anayeeneza ugonjwa wa
dengue baada ya watu watano kugundulika kuumwa na wengine 11 wakionesha dalili
za ugonjwa huo.
Kaimu
mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Dr Christopher Mtamakaya ameyasema hayo jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa dengue na kutoa
tahadhari kwa wananchi kufanya usafi
katika mazingira yao ili kuepuka mazalia ya mbu.
Dr mtamakaya
ambaye pia ni mganga mkuu wa manispaa hiyo amesema watu watatu wamelazwa katika
hospitali ya rufaa ya mawenzi na wengine
watatu wakiwa wamelazwa katika zahanati.
Amesema sampuli za ugonjwa huo zinachukuliwa ili kujua
kama ni ugonjwa hatari wa dengue licha ya kuonesha dalili zote za
ugonjwa huo.
Amesema
tayari ugonjwa huo upo mjini humo na kwamba uwezekano wa kuambukizwa ni mkubwa na amewashauri wananchi kuchukua tahadhari
Post a Comment